Leo hii duniani kote, karibia watu bilioni 10 hutumia simu za mikononi, hapa nimegusia namba wale wanaotumia teknologia ya GSM. GSM ni kifupisho cha Groupe Special mobile. Hii ni teknologia ambayo ilianzishwa mwaka 1982 wakati wa kongamano la wakuu wa mashirika ya posta na mawasiliano (CEPT).
CEPT ni kifupisho cha European Conference of Postal and Telecommunications Administrators. Teknologia hii iko katika kizazi cha pili cha simu za mikononi!, vizazi vingine ni GPRS na EDGE (2.5 Generation), WCDMA, HSPA na LTE(3rd Generation) na LTE-A (4 Generation). Inakadiriwa kuwa karibia asilimia 80 ya simu za mkononi duniani kote hutumia teknologia ya GSM, ndio maana mara nyingi hujulikana kama mfumo wa ulimwengu wa simu za mkononi, yaani kwa kimombo "Global Mobile System". Angalia zaidi hapa kuhusu GSM. Katika makala nyingine, nitaelezea teknologia nyingine za GPRS, EDGE, WCDMA, HSPA, LTE na LTE-A moja baada ya nyingine.
kumbukumbu:
http://cellphones.about.com/od/phoneglossary/g/gsm.htm
0 comments:
Chapisha Maoni