Utangulizi
Unataka kujua jinsi ya kununua vitu kuptia mtandao wa
internet? Tangu kuzaliwa kwa mtandao, watu wamekuwa kununua bidhaa na huduma
online. Internet ni njia kubwa ya kupata vitu ambavyo huwezi kupata katika
maduka ya kawaida au maduka ya rejareja yaliyo karibu nawe karibu nawe, pia
faida nyingine ni kuwa unawez kununua vitu kwa bei nafuu ukilinganisha na
maduka ya kwetu Tanzania.
VITU VYA
KUZINGATIA
·
Kuficha credential zako mf. Neno au namba ya
siri, habari zako binafsi (personal particulars)
Jambo muhimu kukumbuka wakati wa
kununua vitu online ni kuhakikisha unaficha habari zako za kibenki, kwani kuna
wizi mkubwa kwa kutumia mtandao!, watu wamekuwa pia wanafungua tovuti feki ili
kuwalaghai watu!. Pia jaribu kutafuta habari tofauti tofauti kujua athari za kufanya
manunuzi online
·
Huduma za usafirishaji (shipping
services) na waranti.
Pia ni jambo muhimu kuangalia kama kuna huduma
ya usafirishaji, la sivyo, unaweza nunua vitu na bado ukahitajika kutoa gharama
nyingine kuvileta ulipo!. Unapotaka kununua vitu kwa njia ya mtandao, inakubidi
kuangalia tovuti tofauti tofauti kwa
kuwa zinatofautiana kwenye ubora wa huduma, mfano kampuni moja yaweza
uza kitu (item)
bila ya waranti (warranty), lakina nyingine yaweza uza pamoja ya
kutoa waranti ya bidhaa, yaani product
warranty!
NJIA ZINAZOTUMIKA
Credit card
Njia ya kawaida ya kununua vitu online ni kutumia credit
kadi. Hii ni njia kubwa ya kununua vitu online au vitu dukani, ebooks online au
bidhaa ambazo si rahisi kuzipata maduka ya rejareja . Wakati wa kununua kitu na
credit kadi ni lazima kuhakikisha kwamba tovuti ni salama. Kawaida, tovuti
itakuwa na lock kidogo juu yake pia huwa na kiungio cha https badala ya http!.
PayPal
Njia ya pili ya kawaida kwamba watu kununua vitu online ni
kupitia PayPal.
PayPal ni
moja ya makampuni makubwa yanayotuo huduma ya kununua vitu online. Kama tovuti
ni salama na halali, itatoa njia ya PayPal
kama njia ya kuwasilisha malipo. Kufungua akaunti PayPal
ni bure na rahisi sana. tembelea tovuti hii https://registration.paypal.com/na
unaweza kuanza haraka.
eCheck
Moja ya njia ya kawaida kwamba watu kununua kitu online ni
kupitia eCheck.
ECheck inamuwezesha mteja wake kuchukua fedha na kuangalia salio. Akiba katika
akaunti ya eCheck yaweza
kutumika kufanya manunuzi online. Kama unatumia eCheck,
kuwa na uhakika kwamba tovuti ni salama. Njia hii kuchukua muda mrefu sana kwa
mchakato kuliko kadi za credit,
na unaweza kusubiri kwa muda wa hadi siku saba kwa ajili ya malipo kufanyika.
Umuhimu:
Kununua huduma na
bidhaa online ni njia kubwa ya kuokoa fedha
na muda. Ni njia ambayo waweza nunua bidhaa kama za kielektroniki, vitabu na
bidhaa za urembo!.
Angalizo:
Njia hii ya kufanya manunuzi online yafaa kutumika kwa
tahadhari kubwa!, hakikisha unaona kiungio cha https://,
badala ya http//,
pia kiwe na alama ya kofuli kwenye address bar ,
mfano https://www.buyingstuffs.com, vile vile usitumie njia ya manunuzi
isyotambulika/hakikishwa kimataifa au kitaifa! Hakikisha kampuni unayotaka
kununua vitu inatambulika na pia soma masharti na vigezo (terms and
conditions) ili ujue kama uko salama kufanya nao biashara!
Soma zaidi:
http://www.mademan.com/mm/how-buy-things-online.html
# ixzz2RyO2B39l
Kwa maoni na ushauri:
email: dierek2013@gmail.com
0 comments:
Chapisha Maoni