Jiunge kupata chapisho jipya kwa barua pepe!

jua'hatutumi spam!.

Jumapili, 2 Juni 2013

NAMNA BORA YA KUTUMIA SIMU, BILA KUPATA MADHARA MAKUBWA KIAFYA




                                  


Utangulizi

  Simu za mikononi zimemeshakuwa kitu muhimu sana maishani mwetu katika wakati huu ambapo pengine ni dhahiri kumsikia mtu akisema hawezi kutoka bila simu, kumtafuta mtu bila kutumia simu na pia kufanya mambo kadha wa kadha bila kutumia simu za mikononi. Kwa bahati mbaya ama nzuri matumizi ya simu hizi
yameongezeka sana na imefikia hatua hata watoto wadogo wanamiliki vifaa hivi. Hili laweza kuwa jambo zuri kwa maana ya matumizi yake kuwa na tija katika jamii! Simu yaweza tumika kama chanzo cha mapato, kupata taarifa na pia hutusaidia  kutumia muda vizur! Ebu fikiria miaka ya nyuma kabla ya matumizi ya simu hizi,
 ulikuwa ukitaka  kuonana na mtu ni lazima umfuate unakoamini mara nyingi anakuwepo, na kama hayupo ilikulazimu kujaribu mahala pengine na penginge! Lakini uwepo wa vifaa hivi umerahisisha mambo, kiasi kwamba unataka kuonana na mtu
unampigia na kumuuliza kama anapatikana au hapatikani mahala fulan ili uchukue uamuzi sahihi!. Kama ilivyo kawaida, Kila chenye faida kina madhila yake, pia pamoja na uzuri wa vifaa hivi, pia zipo athari mbalimbali kama vile za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiafya. Katika makala hii, nitajikita zaidi katika athari za mbaya kiafya na namna bora ya kupunguza athari hizo.


                                       
MUHUTASARI WA NAMNA SIMU ZINAVYOWASILIANA

Hii ni mahsusi kabisa ili kujua ni nini kinachoendelea, ambacho 
husababisha madhara kwa mtumiaji! Simu hutumia mawimbi ya umeme_sumaku (electromagnetic waves) kuwasiliana na minara (base stations), mawasiliano kati ya mnara na mnara hutumia njia mawimbi hayo (microwave link)! mawimbi haya yote yanatumia frekwensi kubwa (850Mhz-950Mhz), pia yenye nguvu kubwa! mawimbi haya yana uwezo wa kupenya katika mwili wa binadamu na kumsababishia matatizo mbalimbali kama vile ya kansa ya ubongo, pia husababisha vinasaba (DNA) kubadilika (DNA mutation) sababu inayopelekea pia tatizo la kansa! Mtoto ambaye ajazaliwa (foetus) anaweza pia kuathirika kutokana na matumizi ya simu yaliokithiri ya mama yake!



                                                       
                                     
         NAMNA YA KUPUNGUZA ATHARI ZA KIAFYA:

-Epuka matumizi ya muda mrefu ya maongezi kwa simu! Ndio, katika dunia ya leo, vijana tunatumia muda mrefu kuongea na simu, hii ni hatari kwani kadri unavyotumia muda mrefu, mionzi nayo inazidi kuathiri ubongo wako.

KUMBUKA:
  Kutumia headphones hakusaidii kuondoa/kupunguza mionzi, kwa kuwa headphones zita-act kama antennae, hii ni kutokana na mita-bendi ndogo (small wavelengths, range=1nanoMetre) zinazotumika katika mawasiliano haya! Tumia headphones za bomba (air tube headsets) ukiweza.


-Unapolala usiku, weka simu mbali na kichwa! Tuna tabia ya kuweka simu karibu na kichwa wakati wa usiku! Hii ni hatari, kwa kua simu mara nyingi inatafuta mtandao, na pia inawasiliana na mnara mara kwa mara kutumiana taarifa mbalimbali kama za call delivery, sms delivery n.k., hii itakuathiri kiafya!

-Epuka kutumia simu feki! hapa pana changamoto! simu zina kiwango maalumu cha mionzi inayoruhusiwa! kitaalamu, kiwango hiki hujilikana kama Specific Absorption Rate (SAR). Kiwango cha SAR maeneo mengi ulimwenguni kinaanzia 1.6watt/kg-2watt/kg. Unaponunua simu hakikisha simu hiyo ni origino, hii itakusaidia kuepukana na matatizo yaletwayo na simu zitoazo kiwango
kikubwa cha mionzi.

-Matumizi ya simu mbovu! kwa bahati mbaya jambo hili ni gumu kulitambua lakini, wewe mtumiaji unapogundua simu yako ni mbovu, acha kuitumia. simu ikiharibika, yaweza zidisha kiwango cha mionzi inayotoa!

-Pia epuka kutumia/kuongea sana na simu maeneo yenye mawimbi dhaifu (weak BTS signal)kwa kuwa simu yako itatumia nguvu kubwa (High power) ili kufanya mawasiliano na mnara (BTS)! Jambo hili ni hatari kwa afya!





soma zaidi:
                 phone use safetyphone radiations

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Chapisha Maoni