Jiunge kupata chapisho jipya kwa barua pepe!

jua'hatutumi spam!.

Jumanne, 8 Aprili 2014

MP3, MFUMO WA KUIFADHI DATA ZA SAUTI

UTANGULIZI

Mp3/MPEG-I/MPEG-II layer III (Moving Picture Expert Group I/II layer  3)  ni mfumo wa kufomati mafaili ya sauti ya kidigitali. Ni mfumo standadi unaotumika duniani kote kufomati mafaili ya sauti, mfano ni yale ya miziki. Mfumo huu unajulikana kwa kuweza kubadili mafaili yenye saizi kubwa na kuwa na saizi ndogo bila kuathiri sana ubora wa sauti! Kama mnakumbuka vizuri, kipindi cha nyuma CD (Compact Disc) yenye saizi ya 700mb iliweza kuchukua nyimbo chache ambazo zilikuwa zinafomatiwa kwa kutumia mfumo wa PCM (Pulse Code Modulation)! Lakini kuja kwa mfumo wa mp3 kumeweza kupunguza sana saizi ya mafaili ya kidigitali ya sauti (Digital Audio), mfano faili la mfumo wa PCM la 40mb linaweza kugandamizwa (compressed) mpaka likawa na saizi ya 4mb!

NAMNA Mp3 INAVYOFOMATIWA
Faili la kawaida la sauti likiway kwenye mfumo wa digitali linakuwa na data nyingi sana ambazo zilipatikana wakati wa kulibadili kutoka *analogia kwenda digitali. Sasa faili hili la sauti huwa na sampuli nyingi sana, ambazo nyingi zake hazitasikika kabisa katika masikio ya binadamu! Hivyo data hizi ambazo hazitaathiri ubora wa sauti huondolewa kwa kutumia utaalamu wa pyschoacoustics ambao unahusika na kutafiti namna ambavyo sauti onavyopokelewa na kutafsiriwa na masikio! Haraka haraka unaweza kuona namna mfumo unavyohusisha pia saikolojia kufanikisha jambo hili! Kutokana na kupuuza na kuondoa sehemu ya data kutoka kwenye faili, njia hii ni lossy data compression!

HISTORIA FUPI YA MP3
Mfumo wa Mp3 ulianzishwa na kikundi (subgroup) kutoka kundi la Moving Picture Expert Group (MPEG). Kikundi hiki ni MPEG Audio layer I/II/III. Kiliundwa na Fraunhofer society, Hannover University, Technicolor SA, Bell labs, CCETT na wengineo! Kundi la MPEG ndilo lilogundua na kustandadize mfumo wa video mp4 ambao unamika katika kufomati mafaili ya video, pia matangazo mengi ya tv za satellite (satelite tv broadcast) hutumia pia mfumo mp4.

*anologia
          Sauti kwa asili ipo katika mfumo wa analogi!  Anologia ni mfumo ambao mawimbi hubadilika kadiri muda unavyoenda na hayagawanyika (not descrete and not quntable)!

Ref:
      Wikipedia

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Chapisha Maoni