Mambo yamebadilika sana kwenye suala la matumizi ya simu za
mikononi! Vitu ambavyo vilidhaniwa visingewezwa kufanywa kwa kutumia simu za
mikononi vinafanyika sasa, tena kwa
kubonyeza kifungo/batanicha keypad tu! Teknologia mbalimbali zimevumbuliwa
zinazoruhusu kutumia simu kwa kutuma data kwa kasi kubwa!, Ndio, data za
barua-pepe, za kuperuzi tovuti na matumizi mengine ya kisasa ya simu za
mikononi!. Yote haya yamewezekana kwa kutumia teknologia ya GPRS! kirefu chake
ni General Packet Radio Service. Teknologia hii inatumika kwenye kizazi cha
pili cha simu za selula/rununu (2G mobile phones) kuzisaidia kupokea an kutuma
data kwa kasi kubwa!. GPRS inaruhusu simu kuunganishwa muda wote kwenye
mtandao, hivyo kama umetumiwa MMS (MulitiMedia Services), itapakuliwa kwenye
simu yako na kutaarifiwa kuwa una MMS mpya, hivyo huna haja ya kuipakua
unahitajika kubonyeza tu batani kuisoma! Teknologia hii inaweza kutoa kasi ya
32kbps mpaka 48kbps. Sifa nyingine kuu ya teknologia hii ni uwezo wake wa kuruhusu
utumaji na upokeaji wa data hata wakati unaongea na simu! Matumizi ya GPRS
huchajiwa kwa kiwango cha data ulizotumia, sio kwa muda uliotumia kama ilivyo
kwa matumizi ya kawaida ya huduma ya sauti ya simu. Hii teknologia imeziwezesha
simu zinazoitumia kuwa na ufanisi unaokaribia kidogo na ule wa zile zinazotumia
teknologia ya kizazi cha tatu (3G mobile technology)!, ila tofauti kubwa ya 3G
ni uwezo wake wa kuwa na kasi kubwa ya kutuma na kupokea data. Teknologia ya
GPRS iliyoboreshwa inaweza kusapoti huduma mbalimbali kama kuperuzi mtandao,
kutuma barua-pepe, na ujumbe wa picha, sauti na video(MMS), hivyo teknologia
hii yaweza itwa pia 2.5G!
Mchoro unaonyesha namna teknologia ya GPRS inavyoshirikiana na teknologia nyingine kufanikisha mawasiliano ya data
soma zaidi maelezo ya GPRS
0 comments:
Chapisha Maoni