Hii
ni teknolgia ambayo imebuniwa kuuongezea uwezo mfumo wa teknologia ya
mawasiliano ya simu ya GSM (Global Mobile System)! Twaweza kuiita
teknologia hii ya EDGE kama muendelezo wa teknologia ya
GSM iliyoboreshwa kuwezesha usafirishaji wa data kwa kasi kubwa. Teknologia
hii huwezesha kasi hadi ya 384Kbps ukilinganisha na uwezo wa
GSM ambao hutumia kasi ndogo chini ya 60Kbps, ni sahihi kusema EDGE ni mtangulizi wa teknologia ya 3G. Teknologia hii
ilibuniwa mahsusi kwa ajili ya matumizi ya Maltimedia kama
usafirishaji wa video na sauti (Video and audio streaming) kwenye simu
za mikononi! Hii teknologia ilizinduliwa kwa mara ya kwanza nchini
marekani (US) mwaka 2003 na kampuni ya Cingur, ambayo kwa
sasa ni AT&T. Pia imesanifiwa na 3GPP (3rd GENERATION
PARTNERSHIP PROJECT) kama sehemu ya familia ya GSM. angalia zaidi kuhusu 3GPP
picha zime toka: readgsm.blogspot.com, http://www.mechanicalengineeringblog.com/
0 comments:
Chapisha Maoni