Utangulizi
HSPDA ni kifupisho cha High Speed Downlink Packet Access. Hii inamaanisha upatikanaji wa internet yenye kasi kubwa katika upakuaji wa data (high speed downloading), Kumbuka, katika utirikaji wa data, kuna linki mbili, moja ya kwenda mtandaoni ambayo kitaalamu huitwa 'uplink' na nyingine kuja katika kifaa kutoka mtandaoni ambayo huitwa 'downlink'!. 'Uplink'
hutumika wakati kiperuzi (browser) inapotuma maombi kwenda kwenye server! mfano ukitafuta kitu mtandaoni kwa kutumia Google, maneno uliyooandika huongezewa habari maalum (metadata) na kutumwa kwenye server za Google kwa kutumia uplink! na ulichotafuta huletwa kwenye simu/kompyuta yako
kwa kutumia downlink! Teknologia ya HSPDA inakuwezesha kuwa na downlink yenye kasi kubwa sana kuliko ile ya uplink. Teknologia hii inatumika katika 3G kuongeza kasi ya usafirishaji data. Ipo katika standadi za WCDMA. Inaweza kutoa kasi kubwa mara tano zaidi kuliko aina za mwanzo za UMTS, hivyo humruhusu mtumiaji kufaidi kasi kubwa ya upakuaji mtandaoni (High Speed Download). Ina kasi ya mpaka 14.4Mbps ya downlink, na 2Mbps kwenye uplink. Lakini kiuhalisia, mtumiaji anaweza pata kasi ya
400-700Kbps, muda mwingine hadi 1Mbps (data bursts rates).
soma zaidi
https://en.wikipedia.org/wiki/High-Speed_Downlink_Packet_Access
0 comments:
Chapisha Maoni