Utangulizi
Bila shaka umewahi kusikia neno 3G mara kadhaa, likitajwa
mara kwa mara! Pia kama unamiliki/unatumia smart phone,
utaona ikoni (icon) ya 3G! na labda ukabaki ukijiuliza
maana yake/kazi yake ni nini? Kwenye mfululizo wa makala zangu leo nitaelezea teknologia hii ya mawasiliano! Jipange kupata
mambo mazuri. Karibu mpenzi msomaji!
picha imetolewa engineering garage
3G ni nini?
3G ni teknologia ya kizazi cha tatu katika mapinduzi ya mawasiliano ya simu za selula/rununu (cellular mobile phones). 3G kama ilivo ni ufupisho wa Third Generation yaani kizazi cha tatu katika familia ya teknologia hizi. Teknologia hii imebadilisha sana mambo katika ulimwengu wa selula! Mbali na kuongeza kasi ya mawasiliano, pia imewezesha kuongeza ubora wa huduma za mawasiliano kama vile kupiga simu za video, kuangalia video mtandaoni bila kuzipakua na internet ya kasi! Ukiwa na simu yenye uwezo wa #G unaweza kuangalia video kwenye mtandao wa youtube, pia unaweza kuangalia video live kupitia huduma mbalimbali kama DSTV mobile kwa ubora wa hali ya juu! Hii ni teknologia inayoendana na standadi za International Mobile Teknologia-2000 (IMT-2000) kama ilivyoelezwa na International Telecommunications Union (ITU) . Hii ilibuniwa kwa ajili ya huduma za multimedia!
Wachangiaji kwenye ubunifu wa 3G
CDMA2000 -Code Division Multiple Access
TD-SCDMA -Time Division-Synchronous Code-division Multiple Access
W-CDMA (UMTS) - Wideband Code Division Multiple Access
picha
soma zaidi hapa 3G TECHNOLOGY, More information about 3G Tech
0 comments:
Chapisha Maoni